Unawashwa umsogelee rafiki yako umwambie kuhusu Shabani.
“Jamaa anaboa sana, utadhani kampuni ni yake.”
Stori haziishi mpaka tukushitue muda wa kwenda nyumbani; umenogewa kumsema mwenzako.
Kila siku unaongelea kwa nini fulani anajikuta, Juma anachepuka, mwingine ana tabia gani. Ni mengi mabaya waliyonayo hawa watu, eti?
Kwa ulivyo, ni wazi hawa watu leo wakibadilika unaweza hata kukasirika kimoyomoyo. Nahisi utaanza kuchimba ya wengine, ilimradi tupate season 2 ya wewe kuongelea.
Leo ukubali tu, kwamba huwa unajisikia vizuri ukisema wenzako. Hii sio siri tena.
Usiposema ni kama umepatwa na alosto; tukupe kidogo uchangamshe damu, bila hivyo siku haiendi.
Kutokukuonea sana ngoja nikupe ukweli mwingine:
Hata mimi najisikia vizuri kusema watu. Diwani anajisikia vizuri. Jasmini vilevile. Labda ni sehemu ya nature yetu. Tunachotofautiana ni viwango tu.
Kwa nini tumefikia huku sasa?
Kwa sababu wakati mwingine tunajisikia vibaya na hali zetu wenyewe.
Huna kazi unayoipenda. Familia hampendani. Pesa shida. Huna furaha.
Nani anapenda hali kama hiyo, hasa inapokuwa haionekani kuisha kesho?
Hapo ndipo inakuja ile:
Tukifeli wote ni afadhali kuliko nifeli peke yangu.
“Ona yule naye shida tupu. Hahaha”. Ghafla najisikia vizuri na mimi kidogo.
Huko kujisikia vizuri kunatokana na kujifariji kwamba kuna watu wenye hali mbaya kama yako. Kwamba haupo peke yako.
Wasipokuwepo wengine wa kuwaangalia, uhalisia wako unaweza kukutisha. Unaogopa kujitazama usoni na kukubali hali uliyonayo.
Ukisonta vidole kwa wengine, kidogo unasahau yako.
Na tukikosa kuona mabaya kwa watu, wakati mwingine tunayaunda kichwani. Hata kama ni kitu kidogo sana, tutakilazimisha mpaka mtu aonekane ana ubaya fulani. Kwa sababu tunahitaji hiyo dose.
Tunataka kitu kitakachotufanya tujisikie vizuri kuhusu sisi wenyewe bila kubadilisha chochote kuhusu sisi wenyewe.
Rudi ndani.
Ukiwa na amani na hali yako, hutahangaika sana na ya watu.
Shida yako ni nini sasa hivi?
Ikubali. Usikimbie kwa kubugia unga wa kusema wengine kwa shida zao. Hata ukifanya hivyo, hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako.
Kubali shida yako, halafu ibane kuirekebisha kila siku. Njia zipo.
Kadri utakavyoikubali hali yako na kupunguza shida zako, ndivyo utakavyopunguza haja ya kutumia maisha ya wengine kujifariji.
Ya nini ninywe pombe kutuliza mawazo wakati sina mawazo ya kukimbia?
NZ Writes.
Kwenye kikundi chenu bado mnatumia madaftari?
PAMOJARISE inarahisisha uendeshaji wa VIKOBA: michango, mikopo, marejesho, mahesabu na report.
Nani hajalipa? Nani akumbushwe? Nani apigwe faini? Mkopo wa nani umefikia wapi? Huhitaji tena kufuatilia. Mfumo unajua na unawakumbusha wanachama wenyewe.
Miamala ikiwekwa, taarifa zinatumwa. Report ikihitajika, ipo tayari. Mahesabu yote yanafanywa na mfumo.
Mfumo unaofanya kikundi chenu kijiendeshe chenyewe.
👉 Hamishia kikundi chenu PAMOJARISE — tembelea pamojarise.com


