Nishaweka begi langu mgongoni,
Saa kumi na moja imefika—nani abaki kazini?
Na mimi nina kwetu.
Njia kwa kutembea.
Jua linavyong’a wakati wa jioni,
Raha iliyoje.
Nipo peke yangu, kampani inaleta kelele.
Ivi na wengine maisha yao yapo hivi pia?
Kipi kimejaa kichwani mwao muda kama huu?
Mimi nawaza nikaangalie episode nyingine,
Jana nililala saa saba.
Muruha, muruha, pole pole narudi nyumbani kila siku.

