Ally moja ya matajiri vijana jiji Mwanza, anajulikana zaidi kwa kuvutia mabinti wengi kwa kuwa handsome. Ana mke wake Jane ambaye wamekuwa pamoja tangu wakiwa hawana kitu.
Mambo yanabadilika pale biashara yake ilivyoanza kukua na kumfanya kuwa tajiri ghafla.
Sasa ni mtu wa starehe na wanawake kwa sana. Anaongoza kwa kujitapa hakuna mwanamke yoyote anayeweza kumkataa. Uzinzi wake unazidi bila kuficha hata mbele ya mke wake mjamzito.
Kwa tabia yake ya uzinzi wapinzani wake kibishara wanatumia kama njia ya kumpoteza na kuchukua kampuni yake na mali zake zote.
Baada ya kupata taarifa hizi kutoka kwa mke wake ambaye anampigia simu huku akiwa kwenye uchungu wa kujifungua Ally ndio anashituka ujinga wake sasa una hatarisha maisha ya mke wake mjamzito.
Anawasha gari lake kuanza safari kutoka nje ya mji kwenye resort alikokuwa anajivinjari na hawala zake. Anatoka kwa spidi kubwa kumuwahi mke wake huku akikumbuka maneno Daktari wake aliyombambia kuwa mke wake anaweza pata changamoto kwenye kujifungua.
Akiwa njiani kuelekea alipo mke wake katikati ya daraja la busisi kuna gari ambalo linamvamia kwa mbele. Anasimama na kwenye gari wanatoka majambazi waliojifunika nyuso zao wakiwa na siraha, wanamtishia na kumtoa kwenye gari na kumweka kwenye gari lao na kuondoka naye.
…
Siku tano zimepita Ally haonekani alipo. Mke wake ambaye ametokakujifungua watoto mapacha akishirikiana na kaka yake wanamtafuta bila mafanikio yoyote.
Wanapata simu kutoka kwa polisi ambao wanawambia wamefanikiwa kupata gari lake ambapo inasadikika ametekwa na majambazi.
Kwa uhakika lakini bila ushahidi Jane anaanza kuamini hizi zote zitakuwa njama za mshirika wake kibiashara Alford ambaye alimsaliti kupelekea kampuni yake kuchukuliwa na wapinzani wake.
Jane anaamua kutoka mjini Mwanza na kwenda kuishi sengerema kwa siri kwa hofu ya maisha yake na wanae mapacha aliojifungua.
…
Mwaka mmoja umepita.
Hakuna aliyewahi kumuona Ally. Hakuna mwili uliopatikana. Hakuna taarifa yoyote.
Watu wengi wanaamini amekufa.
Jane analazimika kuendelea na maisha yake huku akilea mapacha peke yake.
Lakini siku moja maisha yake yanabadilika tena.
Anakutana ghafla na Alford.
Safari hii Alford hana tabasamu wala maneno ya kirafiki.
Kwa hasira anamtaka Jane amwambie Ally alipo.
Anadai Ally bado yuko hai.
Jane anabaki ameduwaa.
Ikiwa Alford ana uhakika kwamba Ally yuko hai...
Basi swali kubwa linabaki:
ALLY YUKO WAPI?
…


