(Tunarudishwa mwaka mmoja nyuma)
Ni asubuhi karibu na msitu wa Matongo pale ambapo mto Mwesa unatokea wanasikika wanawake wanne wanakatiza wakiwa wamebeba majembe wakiongea Kisukuma.
Bebe nang’o oleyomba John akishihaga
(we nawe unasema John anamsaliti mke wake)
Ghafla mwanamke wa kwanza anapiga kelele
Mayoo
Wenzake wanamuuliza
Ke nang’o?
(Vipi na wewe?)
Anawajibu akiwa na mshituko mkubwa huku akiwasonteshea sehemu kwa mbele
Lolaga he naho
(Tazama pale)
Anaoneka Ally akiwa amelala akiwa amejawa na majeraha makubwa.
Wanawake hao wanapiga kelele wote kwa pamoja
Wooooh
…
(Tunarudi wakati wa sasa mwaka mmoja ukiwa umeshapita)
Tunamwona Ally akiwa Shambani na mzee John.
Inaonekana wapo wakiwa wana assess shamba lao. Ni muda wa mavuno umekaribia.
Katika harakati hizo John anaonekana akipotea kwa kushangaa upande wa pili. kwa mbali kuna mwana mdada mrembo sana ambaye anakatiza
Mara mzee John anampiga begani
Wewe Baraka, nakuona unachungulia tu watoto watu
Mzee John anamwambia kwa rafudhi yake nzito ya kisukuma.
Hahaha, sio hivyo mzee
Ally anajikataliza. Ally hivi sasa huku anaitwa Baraka jina alilopewa na mzee John.
Hahhaha kwahyo unataka kusema ulikuwa unafanya nini
Mzee bwana mimi nilikuwa naangalia mpunga wetu. Mimi kijana mstaarabu si unajua hilo?
Baraka anajitetea.
Wapole wapole hawa ndio huwa misumali. Sipati picha ulikuwaje huko nyuma kabla haujapoteza kumbukumbu.
Ally ambaye sasa ni Baraka inaonekana hana kumbukumbu za nyuma. Mzee John ndio aliyeamua kuishi naye kama mwenyekiti wa kijiji pale alipookolewa.
Sasa hapa twende mashineni kwanza tujue kama tutapata sehemu ya kuhifadhi
Mzee John anabadilisha mada.
John na Ally wanaanza kuondoka.
Wakiwa wanatoka Ally bado anaendelea kumuuliza maswali mbali mbali
Kwahyo hapa tunaweza pata kama magumia mangapi?
…
Sasa wapo mitaa ya mashineni ghafla wanakutana na Mama Zabroni akiwa na mwanamke mwingine.
Mzee John anamsalimia kwa kisukuma.
Ga makanza nzengano
(za mida tena jirani)
Mama Zabroni anamjibu
Mola gete. Nalekobona ulena nzungu wako
(nakuona uko na mzungu wako)
Baraka huwa wanamtania kwamba ni mzungu kulingana na jinsi alivyomweupe pekee kijiji kizima.
Mzee John naye anajibu
No bebe nakubona watwenelwa mwenga wonge. Wahale mwenoyo?
(na wewe naona umetuletea mwinga wa wapi huyu)
Muda huo Baraka anaonekana kuduwaa akimshangaa mwanamke yule ambaye hajawahi kumuona.
Mama Zabroni anamshitua kwa kumwita
Muzungu, unashangaa nini?
Watu wa huku wengi wana rafudhi nzito za kisukuma
Hahahah, mama namshangaa mgeni wetu huyu sijawahi kumwona.
Ally anajiongeresha. Inaonekana wazi amevutiwa naye.
Hahaha na yeye wa mzungu wa mujini kama wewe
Ally ni kama hamsikii Mama Zabroni vile macho yote yamemtoka kwa mdada huyu
Dada karibu sana kisalabi. Naitwa Baraka, mimi ndio mwenyeji wa huku
Anajiuma umauma akiwa anaongea. Ni wazi amevutiwa naye ghafla.
John anampa mkono ili kumsalimia vizuri.
Asante
Kwa majibu ya mkato kama vile anashali naye yule mdada anamjibu.
Mzee John na Mama Zabroni wanaangaliana kwa vibe hii tofauti inayoonekana kati yao.
Huyu ni mtoto wa mtoto wa mamkubwa wa mjini. Amekuja kutusalimia huku.
Mama Zabroni kama namna ya kubadilisha upepo anajazilizia.
Anaitwa Jane au mama wawili.
Mama wawili?! Kwamba ameolewa?
Baraka akiuliza kama amepatamshangao wa ghafla
Hahaha siku nyingine njoo utusamilie kwanza huwa unatupita tu kila siku.
Baraka anaachwa njiani bila kujibiwa shahuku yake.
Mama Zabroni na yule mwanamke wanaondoke wakiwaacha Mzee John na Ally.
Asichokijua Baraka huyu ndiye mke wake Jane ambaye sasa hana kumbukumbu zake tena.


