Nimejitahidi mienendo yangu ikufurahishe bwana,
Lakini upepo wa maisha ya dunia unaniogopesha.
Nahisi naweza pasuka ghafla.
Sina hiyo nguvu ya kuhimili.
Watu wanisifu, ila najiona mnafiki.
Sipo kwenye kiwango cha juu,
Bado najaribu.
Ila uhakika nataka niwe mwema machoni mwako.
Baba nakutegemea wewe,
Wewe ndio wajua udhaifu wangu.
Naomba niimarishe.
Sitaki nipotee zaidi,
Niongoze.

