Kwanza nje ya box ni wapi?
>Toka nje katuletee vitu vilivyo nje ya hili box na sio kutupatia vya humu ndani ya box tulivyo vizoea (na havifanyi kazi)
Sasa ukitoka nje ya box unaenda wapi ukachukue hivyo vitu?
>Humu ndani ya box Kuna nyoka.
Ok, kuna sehemu ukitoka nje ya hili box nakumbuka kulikuwa na fimbo, ngoja niikimbilie tuje tutumie kumuulia huyu nyoka.
Anhaa, kwahiyo ukitoka nje ya box unatakiwa uwe na sehemu ya kwenda?
>Ujanja ni uwe na sehemu ambayo umeshawahi kwenda na unazani kuna kitu unaweza chukua pale kikusaidie kutatua changamoto ulionayo ndani ya box
Sawa sawa, kwahiyo nawezaje fikiria nje ya box?
>Ili uweze kufikiria nje ya box inabidi ujue vitu vingi ambavyo utaweza chagua baadhi utumie kutatua changamoto yako, utakapoishia kujua ndipo uwezo wako wa kuja na vitu vipya utaishia pia.
Kadri unavyojifunza vitu vipya kwa kusoma, kuongea na watu “smart” au kwa namna yoyote inayokujuza vitu ambavyo ulkuwa haujui ndivyo ambavyo unaongeza uwezo wako wa kufikiria nje ya box

